Jumanne, 27 Mei 2014

HARUSI YA MCHUNGAJI ELIAS MBAGATA


 Mchungaji Elias Mbagata akiingia kanisani siku ya harusi
 Mchungaji Marry Makundi akishuka kwenye gari siku ya harusi.
Mchungaji Marry Makundi akiingia kanisani siku ya harusi


 Wachungaji wenzake na Marry Makundi kutoka mikoa mbalimbali wakihudhuria harusi
 Wazazi wa Mchungaji Maryy Makundi wakiwa ndani ya kanisa siku ya harusi
 Mchungaji Elias Mbagata na msindikizaji wake wakiwa wamewasili ndani ya kanisa siku ya harusi


 Mchungaji Mbagata akimfunua shela bibi harusi kuhakikisha kama ni mwenyewe
 Mchungaji Mbagata akifurahi baada ya kufunua shela na kujua kwamba bib harusi ni mwenyewe

 Mchungaji Mbagata akimtunza bibi harusi kwa Tshs 10000
Bibi harusi na bwana harusi wakielekea madhabahuni 
 Bwana harusi na bibi harusi wakiwa wamekaa mbele ya madhabahu
Bwana harusi na bibi harusi wakiwa wakiwa wanasalimiana mbele ya madhabahu
 Bwana harusi akimvalisha pete bibi harusi
Bibi harusi akimvalisha pete bwana harusi 
 Bwana harusi na bibi harusi wakisalimiana baada ya kuvalishana pete
Bwana harusi akisaini cheti cha ndoa 
 Bibi harusi akisaini cheti cha ndoa
 Msindikizaji wa bwana harusi akisaini cheti cha ndoa kama shahidi wa bwana harusi
Msindikizaji wa bibi harusi akisaini cheti cha ndoa kama shahidi wa bibi harusi 
 Bwana harusi na bibi harusi wakiwa kwenye tafrija fupi iliyofanyika nyumbani

 Ndugu, jamaa wakitoa salamu kwa bwana harusi na bibi harusi
 Bibi akipiga picha ya pamoja na bwana na bibi harusi
 Bibi harusi akimpakulia chakula bwana harusi
Wazazi wa bibi harusi wakipiga picha ya pamoja na bwana harusi na bibi harusi 

 Bwana harusi na bibi harusi wakiingia ukumbini
 Bwana harusi na bibi harusi wakikata utepe
 Bwana harusi na bibi harusi wakiwa wamewasili ndani ya ukumbi
 Bwana harusi akimtambulisha bibi harusi kama mke wake rasmi
 Msindikizaji bibi harusi akitoa maelekezo kwa bwana na bibi harusi
 Bwana na bibi harusi wakikata keki
 Bwana na bibi harusi wakilishana keki
 Bwana harusi akiwapa wazazi wa bibi harusi keki

Bwana harusi akiwasilimia wazazi wa bibi harusi baada ya kuwapa keki

 Bibi harusi akiwapa keki wazazi wa bwana harusi

 Bwana na bibi harusi wakinywa shampeni
 Bwana na bibi harusi wakipata chakula
Bwana na bibi harusi wakiwapungia mkono ndugu, jamaa na marafiki


Jumanne, 31 Desemba 2013

EBENEZA AMBAYE NI MTOTO WA TATU WA MCHUNGAJI MBAGATA APATA UBATIZO

Ebeneza wakati akitekeleza ibada ya Ubatizo
Ebeneza akiwa na baba yake mzazi ambaye ni Mchungaji Elias Mbagata katika Kanisa la Injili Afrika wakati alipofika kutoa shukrani kwa hatua ya kufikia Ubatizo.









NYUMBA YA MCHUNGAJI MBAGATA NAYO ILIKUMBWA NA MAFURIKO

Nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Injili Afrika Elias Mbagata ambayo ilikuwa ni moja kati ya nyumba zilizokumbwa na mafuriko yaliyojitokeza kata ya Malolo eneo la Uzunguni.
Baadhi ya watoto walionusurika katika mafuriko hayo ya kata ya Ma yaliyoleta athari kwa zaidi ya watu 102,watoto hawa wanasubiri maji yapungue waende nyumbani kwao katika nyumba zinazoonekana hapo mbele yao.
Mvua ilyosababisha mafuriko hayo ilianza kunyesha majira ya saa moja na nusu asubuhi na kuathiri nyumba kadhaa.


Alhamisi, 5 Desemba 2013

ASANTE KUNIOMBEA.

Naitwa Ebenezer Elias Mbagata ni mtoto wa 3 wa Mchungaji Elias Mbagata.  Wapendwa wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja nanyi kwa kuniombea Mungu amenisaidia kumaliza elimu ya msingi salama katika Shule ya Themi Hill English Medium Academic ambapo pia nimefaulu kwa kiwango kizuri sana katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika kitaifa mwaka huu.  Nimepata Wastani wa Grade  A kwa masomo yote.  Nasubiri kwenda kuanza shule ya sekondari mahalli ambapo Mungu atawaongoza wahusika kunipanga.  Sina budi kumshukuru sana Baba yangu mpendwa Mchungaji Elias Mbagata kwa juhudi zake nyingi pamoja na mambo mengi aliyo nayo kihuduma (na upweke wa kutokuwa na mpendwa wetu Mama yetu aliyetangulia mbele za haki zaidi ya miaka miwili iliyopita) amejitahidi sana kunilipia ada pamoja na kunitimizia mahitaji mengine yote ya muhimu sana kwa miaka yote niliyokuwa shuleni.  Kwa kweli Mungu azidi kumbariki.  Pia mwombeeni kwani bado ana jukumu kubwa la kutusomesha mimi na ndugu zangu Happiness, Deo na Meck pamoja na kutimiza ipasavyo huduma ya BWANA YESU ambayo ndiyo ajira yake. Nawatakia baraka za Mungu.

Ni mimi EBENEZER MBAGATA

Jumapili, 23 Juni 2013

"MWANAMKE ALIYEOZA MKONO AFANYIWA MAOMBEZI NA UPONYAJI"

Janeth Nicholaus (25)mkazi wa Rwanzari Manispaa ya Tabora akionesha mkono wake wa kulia ukiwa tayari umeanza kuoza baada ya kupata ajali ya baiskeli maarufu daladala wakati akitokea nyumbani kwenda Soko kuu la Tabora mjini ajali ambayo ilitokea kwenye makutano ya barabara ya NBC.
Huu ndio mkono wenyewe unavyoendelea kuharibika baada ya kupita hospitali kadhaa hapa Tabora mjini na kushindikana kupona lakini sasa aliamua kufika kwenye huduma ya Maombezi  AGAPE MIRACLE CENTER Mwanzaroad Tabora manispaa
Mchungaji Elias Mbagata akifanyia huduma ya Maombezi Janeth ambaye tayari alianza kukata tamaa na kutaka akatwe mkono huo ili aweze kupata nafuu kutokana na maumivu anayoyapata tangu apate ajali hiyo hadi sasa.
Catherine ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha  SAUT mkoani Tabora akisimama mbele ya waumini AGAPE MIRACLE CENTRE akitoa ushuhuda kuhusu matatizo ya ukosefu wa ada hatua ambayo ilimfanya apate uamuzi wa kutaka kujiua lakini mara baada ya kufika kanisani hapo na kufanyiwa maombi aliweza kufanikiwa kupata ada na sasa anawashukuru waumini waliojitokeza kumpatia msaada huo chini ya usimamizi wa Mchungaji Mbagata.