ASANTE KUNIOMBEA.
Naitwa Ebenezer Elias Mbagata ni mtoto wa 3 wa Mchungaji Elias Mbagata. Wapendwa wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja nanyi kwa kuniombea Mungu amenisaidia kumaliza elimu ya msingi salama katika Shule ya Themi Hill English Medium Academic ambapo pia nimefaulu kwa kiwango kizuri sana katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika kitaifa mwaka huu. Nimepata Wastani wa Grade A kwa masomo yote. Nasubiri kwenda kuanza shule ya sekondari mahalli ambapo Mungu atawaongoza wahusika kunipanga. Sina budi kumshukuru sana Baba yangu mpendwa Mchungaji Elias Mbagata kwa juhudi zake nyingi pamoja na mambo mengi aliyo nayo kihuduma (na upweke wa kutokuwa na mpendwa wetu Mama yetu aliyetangulia mbele za haki zaidi ya miaka miwili iliyopita) amejitahidi sana kunilipia ada pamoja na kunitimizia mahitaji mengine yote ya muhimu sana kwa miaka yote niliyokuwa shuleni. Kwa kweli Mungu azidi kumbariki. Pia mwombeeni kwani bado ana jukumu kubwa la kutusomesha mimi na ndugu zangu Happiness, Deo na Meck pamoja na kutimiza ipasavyo huduma ya BWANA YESU ambayo ndiyo ajira yake. Nawatakia baraka za Mungu.
Ni mimi EBENEZER MBAGATA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni