Jumatano, 19 Juni 2013

HUDUMA YA MCHUNGAJI MBAGATA NI JIBU LA BWANA KWA KANISA LA TANZANIA

Mchungaji Elias Mbagata
 USHUHUDA WA MCHG OSCAR PYUMPA
Kwa jina naitwa Mchungaji Oscar Pyumpa.  Natumika Tutuo wilaya la Sikonge katika Kanisa la Moravian Tanzania Maghaaribi.  

Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya huduma ya Mtumishi wa Mungu Mchungaji Elias Mbagata.  Nimemfahamu kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na awali sikufahamu upana wa maono na hjuduma aliyonayo kwa ajili ya mwili wa Kristo katika mkoa wa Tabora na kwa taifa zima la Tanzania. 

 Huduma kubwa iliyonigusa ni ya mahubiri kwa njia ya redio anayoyatoa kila Jumanne, Alhamisi, na Jumapili kupitia redio VOICE OF TABORA inayosikika katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, na Katavi na kwa sehemu Singida, Ukweli huduma hii imekuwa ya baraaka sana hasa vijijini ambako wahubiri wengi hawafiki, mara nyingi tunakutana na shuhuda za watu wengi waliookoka na kuponywa kupitia vipindi vyake na kwa sababu hiyo Makanisa ya vijijini yanakua na kuongezeka idadi kila siku bila kujali dhehebu. 

 Ukweli niwatie moyo na kuwapongeza wote mnaomwombea na kumtegemeza Mchungaji Mbagata kwani huduma yake ni JIBU LA MUNGU KWA KANISA LA TANZANIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni