Jumapili, 23 Juni 2013

"MWANAMKE ALIYEOZA MKONO AFANYIWA MAOMBEZI NA UPONYAJI"

Janeth Nicholaus (25)mkazi wa Rwanzari Manispaa ya Tabora akionesha mkono wake wa kulia ukiwa tayari umeanza kuoza baada ya kupata ajali ya baiskeli maarufu daladala wakati akitokea nyumbani kwenda Soko kuu la Tabora mjini ajali ambayo ilitokea kwenye makutano ya barabara ya NBC.
Huu ndio mkono wenyewe unavyoendelea kuharibika baada ya kupita hospitali kadhaa hapa Tabora mjini na kushindikana kupona lakini sasa aliamua kufika kwenye huduma ya Maombezi  AGAPE MIRACLE CENTER Mwanzaroad Tabora manispaa
Mchungaji Elias Mbagata akifanyia huduma ya Maombezi Janeth ambaye tayari alianza kukata tamaa na kutaka akatwe mkono huo ili aweze kupata nafuu kutokana na maumivu anayoyapata tangu apate ajali hiyo hadi sasa.
Catherine ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha  SAUT mkoani Tabora akisimama mbele ya waumini AGAPE MIRACLE CENTRE akitoa ushuhuda kuhusu matatizo ya ukosefu wa ada hatua ambayo ilimfanya apate uamuzi wa kutaka kujiua lakini mara baada ya kufika kanisani hapo na kufanyiwa maombi aliweza kufanikiwa kupata ada na sasa anawashukuru waumini waliojitokeza kumpatia msaada huo chini ya usimamizi wa Mchungaji Mbagata.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni