Jumapili, 12 Mei 2013

KANISA LA INJILI AFRIKA TABORA LAOMBEA AMANI TAIFA.

 Baadhi ya waumini katika kanisa la Injili Afrika lilipo Mwanzaroad Tabora mjini wakiombea amani Taifa kufuatia kuwepo kwa vitendo vya kuchoma na kulipua mabomu katika makanisa hapa nchini jambo ambalo limeendelea kuzua hofu kwa baadhi ya waumini.
 Mchungaji Elias Mbagata wa kanisa la Injili Afrika akiongoza ibada hiyo ambayo imefanyika Jumapili ya leo tarehe 12 Mei 2013.
 Mchungaji Elias mbagata alichukua fursa hiyo pia kuwataka waumini wa dini ya kikristo kuondoa dhana ya uadui kati  yao na  waislamu  inayopandikizwa na watu wasiolitakia mema taifa la Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni