Namshukuru sana Mungu kwa jinsi alivyonipigania kupitia huduma ya Mchungaji Elias Mbagata. Tulioana na mke wangu Upendo na kwa muda zaidi ya miaka miwili tangu tuoane hatukupata mtoto. Licha ya kwamba tumeokoka wote kilitusumbua sana kwamba tatizo hili linatokana na nini? ndipo tukamsikia Mchungaji Elias Mbagata akihubiri kwa njia ya redio tukachukua namba zakae za simu, siku moja atukaamua kumtembelea ofosini kwake. Mungu ni wa ajabu sana baada ya kutupa ushauri na kutuombea Mungu ni wa ajabu sana baada ya miezi 6 tu mke wangu akapokea ujauzito na sasa Mungu ni mwema tumejaliwa kupata mtoto wa kiume. Atukuzwe Bwana Yesu na pia Mungu azidi kumbariki Mchungaji Mbagata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni