Jumamosi, 22 Juni 2013

"MWANACHUO ATAKA BARAKA KWENYE PENI ZA KUFANYIA MTIHANI"

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT  Catherine akitokwa na machozi wakati akifanyiwa maombi ya kuhitaji ada ya Chuo ambayo imekuwa ikimuangaisha sana.
Mwanachuo  huyo baada ya  kufanyiwa maombi alifanikiwa  kupata  ada  hiyo  na kuamua kumuandikia  ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani Mchungaji  Elias Mbagata ikiwa  ni  sehemu  ya Ushuhuda wake:-

"Bwana  YESU asifiwe!Ninaamin wewe ni mzima wa afya hata mimi pia mwanao ni mzima kabisa na ninaendelea vzuri,jana  baada  ya  ibada nishndwa kukuona  kwasababu nliona kama ulikuwa unakazi fulan,MUNGU aendelee kukutia nguvu katka huduma kwan ninakuombea sana ili ufankiwe zaid katika huduma hiyo uliyokuwa nayo,kesho ninaomba kuja na peni zangu za mtihan ili ziwe na baraka pia naleta na risit ya ada nashukuru sana kwan kwa maombi yenu nitafanya mtihan ila wengne hawatafanya kwasababu ya kutolipa ada,jion njema".

Huu ndio ushuhuda wa mwanachuo huyu ambaye alipata ada ya shilingi laki moja ambayo alichangiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni